Huwezi kusikiliza tena

Mgogoro wa Burundi, Tanzania yazungumza

Muungano wa Afrika, AU, umetangaza kwamba umejiandaa kuwatuma zaidi ya wanajeshi 5,000 wa kudumisha amani nchini Burundi.

Hayo ni katika juhudi za kuwalinda raia, huku mzozo wa kisiasa nchini humo ukiendelea kuzidi.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya muungano huo kuamua kuwatuma wanajeshi katika nchi mwanachama, na huku bila nchi hiyo kuridhia kuwapokea wanajeshi hao.

Burundi leo imetangaza kwamba haitaviruhusu vikosi vyovyote pasipo idhini yake.

Hayo yakiendelea, nchi jirani ya Tanzania imependekeza mpango wake wenye lengo la kuleta amani