85 watoweka baada ya maporomoko China

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption 85 hawajulikani waliko baada ya maporomoko

Zaidi ya wakoaji 1000 wanatafuta manusura kusini mwa China siku moja baada ya maporomoko ya ardhi kuangusha nyumba 33 katika mji wa Shenzhen .

Watu saba wameokolewa lakini wengine 85 bado hawajulikani waliko baada ya tope kuporomoka katika mtaa mmoja wa kiviwanda katika mji wa Shenzhen.

Takriban watu 900 walihamishwa kabla ya kutokea kwa maporomoko hayo.

Waokoaji wanaotumia tinga tinga na mbwa wa kunusa wanasema kuwa wamepata dalili za watu walio hai sehemu kadha.

Haki miliki ya picha Xinhua
Image caption Takriban watu 900 walihamishwa kabla ya kutokea kwa maporomoko hayo.

Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa udongo huo ulikuwa umejazwa eneo moja kinyume cha sheria.

Udongo huo unatokana na timbo inayotumika kusaga mawe ya ujenzi na pia jaa ya mabaki ya ujenzi.

Mji wa Shenzhen ni moja kati ya miji mikubwa zaidi nchini China mbali na kuwa mji mkubwa zaidi kiviwanda.

Poromoko hilo la ardhi liliathiri takriban mita laki nne mraba likifunika ardhi na mita 10 ya udongo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Udongo huo unatokana na timbo inayotumika kusaga mawe ya ujenzi na pia jaa ya mabaki ya ujenzi.

Shirika la habari la taifa Xinhua limesema maporomoko hayo yalisababisha mlipuko katika kituo kimoja cha mfereji wa gesi ya kupikia.

Takriban mita mia 400 ya mifereji ya gesi imeharibiwa.