Wapiga kura wapinga sheria ya jinsia moja

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiga kura wapinga ndoa ya jinsia moja

Wapiga kura nchini Slovenia wamekataa sheria ambayo itawaruhusu wapenzi wa jinsia moja kufunga ndoa na kupanga watoto.

Takriban theluthi mbili ya wapiga kura walikataa mswada huo ambao uliidhinishwa mwezi machi.

Mswada huo ulisema kuwa ndoa ni kati na watu wawili wazima badala ya kati ya mwanamume na mwanamke.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Takriban theluthi mbili ya wapiga kura walikataa mswada huo ambao uliidhinishwa mwezi machi.

Wanaharakati wanaowatetea watoto ambao wamekuwa wakipinga mswada huo wakisema kuwa matokeo hayo ni ushindi kwa watoto wao.

Lakini wale wanaotetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanasema kuwa licha ya matokeo hayo kuna mafanikio kwa sababu suala hilo limekuwa likijadiliwa kwa umma.