IAAF ilipanga njama kuficha wanariadha wadanganyifu

Haki miliki ya picha Istock
Image caption IAAF ilipanga njama kuficha wanariadha wadanganyifu

BBC imepata ushahidi kuhusu mpango wa kisiri ndani ya shirikisho la riadha duniani kuchelewesha kutangazwa kwa majina ya wanaridha waliopatikana na hatia ya kutumia madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini hadi wakati wa mashindano ya olimpiki yalioandaliwa mjini Moscow Urusi mwaka 2013.

Mpango huo umebainika baada ya barua pepe iliyotumwa na naibu katibu mkuu wa IAAF Nick Davis kupatikana.

Image caption IAAF iliwapiga marufuku wanariadha 16 wa Urusi miezi minne baada ya mashindano hayo

Kwenye barua hiyo, aliyokuwa amemuandikia Papa Massata Diack ,uwezo wa Urusi kuandaa mashindano hayo ulitiliwa shaka kufuatia kuwepo kwa visa vingi vya matumizi ya dawa ya kuongeza nguvu nchini humo.

Massata Diack, aliyekuwa mshauri wa mauzo katika shirikisho la riadha duniani IAAF ni mwanaye aliyekuwa rais wakati huo IAAF Lamine Diack.

Davies aliandika kwamba alihitaji ‘kuketi’ na timu ya kupambana na utumizi wa madawa ya kuongeza nguvu mwilini ili kujadili ‘siri za Kirusi zilizofichwa ".

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Massata Diack, aliyekuwa mshauri wa mauzo katika shirikisho la riadha duniani IAAF ni mwanaye aliyekuwa rais wakati huo IAAF Lamine Diack.

Davies aidha alipendekeza kuwa IAAF ‘ilihitajika kuwa werevu’ kuhusu swala la kuchapisha majina ya wanariadha waliopatikana na hatia.

IAAF iliwapiga marufuku wanariadha 16 wa Urusi miezi minne baada ya mashindano hayo, ambayo nchi hiyo iliongoza kwenye jedwali la nishani.