Mbunge afariki katika kikao cha bunge Kuwait

Image caption Mbunge afariki katika kikao cha bunge Kuwait

Mbunge mmoja nchini Kuwait amefariki katika kikao cha bunge.

Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii imeonyesha mbunge huyo bwana Nabil al-Fadl aliye na umri wa miaka 65 akianguka kwa ghafla kutoka kwenye kiti chake.

Wabunge walimzingira, kisha waziri wa afya (Dr Ali al-Obaidi) akijaribu kumtibu hadi wakati madaktari walipowasili.

Marehemu bwana Al-Fadl -- ambaye alikuwa ni mwandishi wa habari alikuwa maarufu kwa kutumia jarida lake kuwaasa wabunge wenza na hata wakati mwengine kuwakashifu.

Aidha Al-Fadl alifahamika zaidi kwa kuwakaripia waasi wa kiislamu ambao aliwashambulia kwa maneno makali .

Wakati mmoja aliwashangaza wasomaji wake alipoitaka serikali iondoe mara moja marufuku ya uuzaji wa pombe na maeneo ya burudani.