Urusi kumkamata M.Khodorkovsky

Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Mikhail Khodorkovsky

Mtawala wa zamani na mfanya biashara mashuhuri mwenye ushawishi wa kisiasa , Mikhail Khodorkovsky, ameiambia BBC kwamba uamuzi wa mahakama nchini Urusi kutoa hati ya kumkamata imetawaliwa na utashi wa kisiasa.

Bwana Khodorkovsky, ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni,na kutumia kipindi cha miaka kumi jela kwa tuhuma za ufisadi na anadai kwamba hati hiyo ina mpango wa kumnyamazisha.

Kwa sasa mfanya biashara huyo anamlaumu Rais Putin kwa kumgeuka kwasababu ya yeye Mikhail kuonekana anaunga mkono harakati za upande wa upinzani . Anakielezea chama tawala kwamba kina hasira kali juu yake .

Katika tamko la awali alieleza kwamba kesi hiyo ilikwisha tatuliwa.

Naye msemaji wa rais Putin,amesema kwamba mashtaka ya Mikhail ni ya jinai na kuongeza kwamba hakuna utata wowote baina ya msamaha wa rais uliotolewa miaka miwili iliyopita na hati hiyo ya sasa ya kukamatwa kwake.