Jeshi la Nigeria lilizika 300 katika makaburi ya halaiki

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Majeshi ya Nigeria yalizika wasilamu wa Shia katika makaburi ya halaiki -Human Rights Watch

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch limelaumu jeshi la Nigeria kwa kuwaua mamia ya Waislamu wa dhehebu la Shia Kaskazini mwa Nigeria.

Jeshi la Nigeria lilifanya oparesheni kadhaa katika mji wa Zaria kufuatia kile ilichotaja kama njama ya kutaka kumuua mkuu wa jeshi nchini humo.

Human Rights Watch wamewalaumu wanajeshi wa Nigeria kwa kufyatulia risasi watoto wadogo wasio na silaha baada ya watoto hao kuzuia msafara wa kijeshi.

Ingawa wanajeshi wanadai hilo lililkuwa jaribio la kumwua mkuu wa jeshi, Human Rights Watch linasema maelezo ya jeshi hayalingani na ukweli halisi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Human Right Watch wanasema zaidi ya watu 300 waliuawa katika mashambulizi hayo.

Kulingana na shirika hilo la kutetea haki za kibinadamu kilichotokea baada ya hapo ni mashambulizi kadhaa dhidi ya Washia katika mji huo.

Human Right Watch wanasema zaidi ya watu 300 waliuawa katika mashambulizi hayo.

Shirika hilo linasema kuwa maelezo yaliyoko kwa sasa ni kuwa jeshi lililipiza kisasi kwa ukatili zaidi au sio lilishambulia eneo hilo kwa lenga la kuwanyanyasa Washia makusudi.

Jeshi limekanusha kuwa mamia waliuawa na limesema ukweli utatambuliwa baada ya uchunguzi kamili kufanywa.

Image caption Kiongozi wa washia nchini Nigeria

Mauaji hayo yalisababisha maandamano katika miji kadhaa kote nchini na kuenea hadi Iran na India.

Mmoja wa viongozi wa kidini maarufu nchini Nigeria amesema kuwa huenda mashambulizi hayo yakazusha maasi mapya nchini humo.

Jeshi la Nigeria kwa sasa linapambana vikali na waasi wa Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa nchi.

Kundi hilo la waasi wa Kiislamu limewaua maelfu ya watu katika juhudi za kubuni Himaya ya Kiislamu.