Familia ya waislamu yakatazwa kwenda Disney

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mahmood alikuwa akisafiri na kakake na wanao 9 walikuwa wamepanga kuzuru California Kusini wanakoishi jamaa zao kisha watembelee maeneo ya burudani ya Disney.

Shinikizo linazidi kushika kasi nchini Uingereza kufuatia hatua ya maafisa wa usafiri nchini Marekani kuwanyima idhini ya kusafiri familia moja ya Waislamu waliokuwa wanataka kwenda Los Angeles Marekani.

Familia hiyo ya watu 11 kutoka eneo la Walthamstow walikuwa wamepanga kwenda Disneyland lakini walikatazwa kuabiri ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Gatwick Disemba tarehe 15.

Mohammad Tariq Mahmood na familia yake hawakupewa sababu yeyote na maafisa wa usalama katika uwanja huo.

Mahmood alikuwa akisafiri na kakake na wanao 9 walikuwa wamepanga kuzuru California Kusini wanakoishi jamaa zao kisha watembelee maeneo ya burudani ya Disney.

Hata hivyo walipofika katika uwanja a ndege wa Gatwick maafisa wa usalama waliwaeleza hatua hiyo iliyochukuliwa na maafisa wa usalama wa Marekani.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption ''Utawaelezaje watoto kuwa hatukuruhusiwa kusafiri kwa sababu sisi ni waislamu ? ''Wataelewaje ? aliuliza bwana Mahmood

''Mmoja kati maafisa wa kusimamia mipaka aliniambia kuwa hamtaruhusiwa kuingia katika ndege hiyo ya kwenda Marekani''

''Wakati huo tulikuwa tunakaribia kukamilisha upekuzi ilituingie ndani ya ndege, tukamrishwa kuondoka kwenye foleni''

''Niliabika sana ''alisema bwana Mahmood.

''Japo nilikuwa nimewahi kuzungumzia swala la ubaguzi dhidi ya Waislamu kote nchini Uingereza sikujua kuwa itafikia siku ambayo swala hilo litaniathiri mimi na familia yangu''

Walielezwa kuwa hawatarejeshewa gharama yao ya pauni elfu 9,000.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption UK: Familia ya waislamu yakatazwa kwenda Marekani

Vilevile walielezwa warejeshe kila kitu walichokinunua katika maduka yasiyotozwa kodi kabla ya kufurushwa nje ya uwanja huo.

''Utawaelezaje watoto kuwa hatukuruhusiwa kusafiri kwa sababu sisi ni waislamu ?

''Wataelewaje ? aliuliza bwana Mahmood

Waziri wa uhamiaji wa Uingereza, James Brokenshire aliahidi kuchunguza swala hilo.

Mbunge wa eneo wanakotoka la Walthamstow bi Stella Creasy amemtaka waziri mkuu kutoa ripoti rasmi bungeni kwanini Marekani imekuwa ikiwazuia waingereza waislamu kutoingia Marekani bila kutoa sababu yeyote ?