Mzoga wa nyangumi wapatikana ufukweni

Image caption Mzoga wa nyangumi wapatikana ufukweni

Mzoga wa nyangumi umepatikana ufukweni nje ya mji Capetown Afrika Kusini.

Mzoga huo unaaminika kusombwa na maji ya bahari na kukwama kwenye mwamba.

Haijabainika kilichosababisha kifo cha nyangumi huyo.

Image caption Haijabainika kilichosababisha kifo cha nyangumi huyo.

Mwanidhi wa BBC aliyeko huko Pumza Fihlani anasema kuwa maafisa wa afya wa umma wametangaza kuwa ufukwe huo utafungwa kwa umma leo, ilikufanikisha shughuli ya kuondoa mzoga huo uliowavutia halaiki ya watu mapema leo.