Wageni waonywa watahadhari mjini Beijing

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Balozi za Marekani na Uingereza zimetoa tahadhari kwa raia wake.

Polisi nchini china wametoa tahadhari ya usalama kuhusu kuwepo vitisho vya mashambulizi dhidi ya raia wa nchi za magharibi katika moja ya mitaa yenye shughuli nyingi mjini Beijing.

Balozi za Marekani na Uingereza zimetoa tahadhari kwa raia wake.

Polisi waliojihami wametumwa kwenye maduka katika wilaya ya Sanlitun ambapo miezi minne iliyopita kijana mmoja aliyekuwa na kisu alimuua mwanamke mchina na kumjeruhi mwenzake raia wa Ufaransa.

Image caption Balozi za Marekani na Uingereza zimetoa tahadhari kwa raia wake.

Serikali ya Ufaransa na Australia pia zimetangaza hali ya tahadhari kwa raia wao walioko China.

Maafisa wa usalama mjini humo wametoa tahadhari ya manjano, hii ni tahadhari ya pili katika mfumo wao wenye viwangi vinne vya tahadhari.

Hii inamaanisha kuwa kutakuwepo na upekuzi zaidi mbali na doria ya polisi wa kawaida waliojihami kwa silaha.

Image caption Sanlitun lililoko katika wilaya ya Chaoyang lina idadi kubwa ya mabaa na migahawa ambayo ni maarufu sana na raia wa kigeni.

Wenyeji wa Sanlitun wameshuhudia ongezeko maradufu ya idadi ya polisi wanaoshika doria nje ya majengo yenye maduka makubwa makubwa ya jumla.

Eneo la Sanlitun lililoko katika wilaya ya Chaoyang lina idadi kubwa ya mabaa na migahawa ambayo ni maarufu sana na raia wa kigeni.