Mhamiaji ashinda dola laki 4 Uhispania

Image caption Mhamiaji ashinda dola laki 4 Uhispania

Mhamiaji mmoja raia wa Senegal ambaye hana kazi ameshinda jumla ya dola 400,000 katika mchezo wa krismasi wa bahati nasibu nchini Uhispania.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 35 na mkewe waliokolewa na walinzi wa pwani ya Uhispania wakati walifunga safari kupitia bahari ya Morocco miaka minane iliyopita.

Tangu siku hiyo wamekuwa wakiishi kwa chini ya dola tano kwa siku wakiwa wafanyikazi wa shambani.

Sasa imeibuka kuwa alikuwa mmoja wa watu 1600 waliopata bahati ya kushinda.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 35 na mkewe waliokolewa na walinzi wa pwani ya Uhispania wakati walifunga safari kupitia bahari ya Morocco

Ngagne ni mmoja kati ya watu 1600 walioshindi walionunua sehemu ya kapu hilo la pauni bilioni 1.6.

Mchezo huo wa bahati nasibu wa El Gordo (aliyenenepa), hufanyika kila mwaka.