Perera wa Sri Lanka akabiliwa na marufuku

Perera
Image caption Perera hataweza kuchezea Sri Lanka katika Kombe la Dunia la T20

Mchezaji wa timu ya kriketi ya Sri Lanka Kusal Perera anakabiliwa na hatari ya kupigwa marufuku miaka minne baada ya kugunduliwa ametumia dawa zilizoharamishwa.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 25 aligunduliwa baada ya kupimwa Oktoba.

Aliondolewa kutoka kwenye timu iliyokuwa ziarani New Zealand mapema mwezi huu.

Waziri wa michezo wa Sri Lanka Dayasiri Jayasekara amesema taifa hilo litakata rufaa iwapo atazuiwa kucheza.

Awali, Jayasekara alikuwa amedai matokeo hayo ni njama ya kumzuia Perera kucheza katika Kombe la Dunia la T20 mwaka ujao.