Kamanda wa Pakistan ziarani Afghanistan

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kamanda wa Pakistan ziarani Afghanistan

Kamanda mkuu wa jeshi la Pakistan, Jenerali Raheel Sharif, amewasili katika mji mkuu wa Afghanistan - Kabul, ili kushauriana na rais wa nchi hiyo, Ashraf Ghani, pamoja na viongozi wengine wa kisisa na kijeshi.

Mazungumzo hayo yataangazia kurejelewa tena kwa mazungumzo ya amani nchini Afghanistan.

Mazungumzo ya awali yalikwama mapema mwaka huu, baada ya wanamgambo wa Taliban, kutangaza kuwa kinara wao Mullah Omar, alikuwa amekufa miaka miwili iliyopita.

Afghanistan inatafuta uungwaji mkono kutoka Pakistan, kama hatua muhimu ya kurudi tena katika meza ya mduara na wanamgambo wa Taliban.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mazungumzo hayo yataangazia kurejelewa tena kwa mazungumzo ya amani nchini Afghanistan.

Msemaji wa jenerali Sharif, anasema kuwa anaingia katika mazungumzo hayo, kwa moyo mweupe na wa ujasiri.

Na sasa msikilizaji nakuachia makala kutoka Tanzania kuhusu matukio makubwa yaliyofanyika mwaka huu wa 2015.