Boko Haram lawaua 14 Nigeria

Haki miliki ya picha Boko Haram video
Image caption Boko Haram laua 14 Nigeria

Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, zinasema kuwa takriban watu 14 wameuwawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa Boko Haram.

Walioshuhudia wanasema kuwa watu wenye silaha waliingia katika kijiji cha Kimba kilichoko katika jimbo la Borno wakitumia baiskeli.

Walianza kuwamiminia risasi wakaazi huku wakiteketeza nyumba zao.

Siku moja kabla ya shambulizi hilo, rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, aliiambia BBC kuwa Nigeria kimsingi imeshinda vita dhidi ya wanamgambo hao wa Boko Haram.

Aidha Rais Buhari alisema changamoto tu iliyopo ni kitovu tu cha Boko Haram katika jimbo la Borno mahali shambulio hilo lilitokea siku ya Ijumaa.