Mshambuliaji wa kwanza wa Paris azikwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Anadhaniwa kuwa wa kwanza kati ya washambuliaji kuzikwa

Maafisa mjini Paris wanasema kuwa mmoja wa watu ambao wanatuhumiwa kutekeleza mauaji ya kigaidi katika mji mkuu wa Ufaransa Paris mwezi uliopita amezikwa katika kaburi iliyofichika katika kitongoji kimoji jiji humo .

Wanasema kuwa Samy Amimour alizikwa siku ya Alhamisi katika kitongoji cha Paris ( Seine Saint Denis ) ambapo wazazi wake wanaishi .

Amimour alikuwa mmoja wa wavamizi watatu walioshambulia tamasha la muziki katika ukumbi wa Bataclan ambao watu 90 walipigwa risasi na kuuawa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ukumbi wa Bataclan ambapo watu 90 walipigwa risasi na kuuawa

Anadhaniwa kuwa wa kwanza kati ya washambuliaji kuzikwa .

Jumla ya watu mia moja na thelathini alikufa katika mashambulizi ya Paris Novemba tarehe 13.