Mlinzi wa Osama bin Laden afariki dunia

Bahri
Image caption Al Bahri aliwahi kuzuiliwa Guantanamo

Taarifa kutoka Yemen zinasema aliyekuwa mlinzi wa Osama Bin Laden, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Vyanzo vya habari vya kitabibu vimeiambia BBC kwamba Nasser al Bahri ambaye pia alikuwa akijulikana kama Abu Jandal alifariki siku ya Jumamosi, katika Hospitali iliyoko kwenye mji wa Mukalla kusini mwa Yemen.

Alirudi nchini humo mwishoni mwa mwaka 2008, baada ya kuachiliwa kutoka katika kizuizi alichowekewa na Marekani huko Guantanamo.

Al Bahri alijulikana kuhusika na mashambulizi yaliyofanywa na mtandao wa kigaidi katika miaka ya 90, katika nchi za Afghanistan, Somalia na Bosnia.