Stars Wars yavunja rekodi ya kuvuna $1bn

Star Wars Haki miliki ya picha Disneylucasfilm
Image caption Filamu ya The Force Awakens ilionyeshwa mara ya kwanza 14 Desemba

Filamu mpya ya Star Wars: The Force Awakens imevunja rekodi na kuwa filamu iliyozoa $1bn (£674m) kwa kasi zaidi duniani.

Filamu hiyo ya JJ Abrams imefikia pesa hizo katika muda wa siku 12, na kuvunja rekodi ya awali ya siku 13 iliyowekwa na Jurassic World mwezi Juni.

Lakini ingawa Jurassic World ilikuwa na nafuu ya kuonyeshwa Uchina pia, filamu ya The Force Awakens bado haijaanza kuonyeshwa huko.

Star Wars pia iliandikisha historia ya kupata mauzo zaidi ya tiketi Siku ya Krismasi nchini Marekani kwa kuuza $49.3m (£33.2m).

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Filamu ya The Force Awakens imezua msisimko mkubwa duniani, hapa ni msemaji wa White House Josh Earnest na baadhi ya wahusika

Filamu hiyo iliuza $153.5m (£103.5m) nchini Marekani wikendi yake ya pili na kufikisha jumla ya mauzo hako hadi $544.6m (£367m).

Filamu hiyo ya The Force Awakens ndiyo ya saba katika mwendelezo wa filamu za Stars Wars na lieonyeshwa kwa mara ya kwanza Los Angeles tarehe 14 Desemba.

Filamu hiyo imeshirikisha waigizaji kutoka kwa filamu ya kwanza kabisa Harrison Ford, Mark Hamill na Carrie Fisher na wageni wakiwemo John Boyega na Daisy Ridley.