Aliyetumia utajiri kukwepa jela akamatwa Mexico

Image caption Mmarekani asiyejua jema au baya akamatwa Mexico

Kijana kutoka jimbo la Texas Marekani ambaye anadaiwa kukwepa kwenda jela baada ya kusababisha vifo vya watu wanne aliposababisha ajali alipokuwa akiendesha gari akiwa mlevi amekamatwa nchini Mexico.

Yamkini kijana huyo alikwepa kifungo baada ya mawakili wake kuishawishi mahakama kuwa alikuwa ni tajiri wa kupindukia na kuwa hakuweza kutambua mema au mabaya.

Ethan Couch aliyejulikana kama kijana wa ' affluenza ' aliwagonga watu wanne akiwa amelewa chopi mwaka wa 2013.

Couch alikuwa anatumikia kifungo cha nyumbani cha miaka kumi.

Hata hivyo yeye na mamake Tonya wanaosemekana kuwa matajiri sana walitoweka mapema mwezi huu.

Wanadaiwa kuwekwa chini ya ulinzi mkali katika pwani ya Magharibi mwa Mexico,Puerto Vallarta .

Amri ya kukamatwa kwa Couch ilitolewa mapema mwezi huu baada ya kukosa kufika kufika kwa afisa wa magereza wa kurekebisha tabia.

Image caption Yamkini kijana huyo alikwepa kifungo baada ya mawakili wake kuishawishi mahakama kuwa alikuwa ni tajiri wa kupindukia na kuwa hakuweza kutambua mema au mabaya.

Couch alijulikana kwa utetezi wake usio wa kawaida, alipodai kuwa malezi yake katika familia tajiri yalimnyima uwezo wa kubaini mema au mabaya.

Maafisa katika jimbo la Tarrant waliwafahamisha maafisa katika afisi ya mwanasheria mkuu katika jimbo la Texas Marekani kuwa walimkamata kijana huyo alipokuwa Puerto Vallarta .

Afisa mkuu wa jimbo hilo la Tarrant , Dee Anderson, amesema anaamini Couch na mama yake walikimbia mwishoni mwa mwezi Novemba baada ya video kuenea ikimwonesha Couch akijiburudisha katika sherehe moja iliyokuwa ni vileo.

Kulingana na kauli ya mahakama Couch alipigwa marufuku ya kunywa pombe kwa kipindi cha miaka 10.

Na akipatikana akiwa mlevi angeweza kuhukumiwa upya kifungo cha miaka 10 gerezani.