Njama ya kuokoa Diendere yatibuka Burkina Faso

Haki miliki ya picha
Image caption Maafisa mjini Ouagadougou wanasema kuwa serikali ilitibua njama ya kumuachilia huru jenerali Gilbert Diendere.

Takriban maafisa 20 wa kijeshi wamekamatwa nchini Burkina Faso baada ya serikali kutibua njama ya kumuachilia huru kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwezi Septemba.

Maafisa mjini Ouagadougou wanasema kuwa serikali ilitibua njama ya kumuachilia huru jenerali Gilbert Diendere.

Vyanzo vya afisi ya waziri mkuu Isaac Zida vinasema kuwa , maafisa hao walikuwa na nia ya kuwaachilia huru washukiwa wote wa mapinduzi mbali na kukirejesha kikosi hicho cha kumlinda rais kilichopigwa marufuku kufuatia jaribio hilo la mapinduzi.

Aliachia madaraka baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa umma na viongozi wa kikanda.

Kikosi chake kilichokuwa kikimlinda rais kimehusishwa na njama hiyo mbali na madai mengine mengi ya ukiukaji wa sheria na kwa ukatili uliotekelezwa wakati wa utawala wa rais Compaoré.

Njama hiyo imetibuka katika siku ambayo taifa hilo linamtarajia rais mpya kuchukua hatamu leo.

Rais huyo mpya Roch Marc Christian Kabore amesema kuwa ''sheria itafwata mkondo wake''

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jenerali Diendere na Compaore, wanakabiliwa na tuhuma za mauji ya rais wa zamani wa taifa hilo Thomas Sankara

Waziri mkuu Zida amesema ''Tumewatia mbaroni ilikutoa ilani kuwa njama kama hiyo hainabudi ila kutibuka''

Jenerali Diendere na Compaore, wanakabiliwa na tuhuma za mauji ya rais wa zamani wa taifa hilo Thomas Sankara.

Wamekanusha madai dhidi yao.