Wavutaji sigara waonywa wasipuuze kikohozi

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Wavutaji sigara waonywa wasipuuze kikohozi

Wavuta wa sigara wameshauriwa wasipuuze kikohozi kwani inaweza kuwa ishara ya ugonjwa mbaya zaidi unaoweza kudhoofisha na hata kuhatarisha maisha ya wavutaji sigara.

Katika kampeini mpya ya kuhamasisha wavutaji sigara kuhusu athari za uvutaji sigara kwa afya yao, idara ya afya ya umma nchini Uingereza inaonya kuwa wavutaji sigara wengi hawajui hatari ya ugonjwa sugu wa pingamizi ya mapafu ama chronic obstructive pulmonary disease (COPD).

COPD, ainalaumiwa kwa kusababisha mishipa ya hewa kuwa nyembamba mno na hata kufanya wahasiriwa kukosa pumzi wanapotekeleza majukumu mepesi kama kupanda ama hata kushuka ngazi.

Takwimu zinaonyesha watu zaidi ya milioni moja nchini Uingereza wanaishi na hali hiyo.

Vilevile visa 9 kati ya 10 vinavyopatikana vinasababishwa na sigara.

COPD ni mwavuli unaoashiria jumla ya maradhi yanayotokana na kudhoofika kwa mapafu ikiwa .

Hakuna tiba

Watu wenye ugonjwa huu wanamatatizo ya kupumua, hasa kutokana na kupungua kwa uwezo wao wa kupumua na uharibifu wa mapafu.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Vilevile visa 9 kati ya 10 vinavyopatikana vinasababishwa na uvutaji sigara.

Dalili ya kawaida ni pamoja na kukosa pumzi hawa wakati unapotekeleza majukumu mepesi, kikohozi kisichosikia dawa na maambukizi ya mara kwa mara kifua.

Idara ya Afya ya Umma nchini Uingereza (PHE) imeanzisha kampeini hii mpya yenye matangazo na kuonya kuwa wavuta wachukulie kikohozi kuwa dalili mbaya na dalili ya kwanza wa maambukizi mabaya ya mapafu.

Hakuna tiba ya maradhi haya,ila iwapo mvutaji ataacha kuvuta sigara,mipango lengwa ya zoezi na dawa zinaweza kupunguza kasi ya maambukizi ya COPD.

Ili kuongeza uelewa juu ya ugonjwa huo, PHE imeandaa filamu fupi inayotumiwa katika kampeini hiyo kwenye mitandao.

Filamu hiyo inamhusisha bingwa wa zamani wa Olimpiki Iwan Thomas, ambaye mamake alipatikana hivi karibuni na ugonjwa wa COPD.

Thomas anafanya majaribio na wavutaji sigara kuona iwapo COPD inaweza kupunguzwa miongoni mwa wavutaji sigara.

Image caption Takwimu zinaonyesha watu zaidi ya milioni moja nchini Uingereza wanaishi na hali hiyo.

Thomas alisema: "Sijawahi kueleweka kikamilifu COPD au athari yake katika maisha ya kila siku, lakini wakati mambo rahisi kama kupanda ngazi, na kutengeneza kikombe cha chai au kutembea kutoka kituo cha mabasi inaanza kuwa vigumu kwangu ndipo ilinifanya nikatahamaki.''

'Mwaka wa kuacha sigara'

"Baada ya uvutaji sigara wa miaka mingi , mamangu mzazi ameamua kuwa mwaka wa 2016 ndio mwaka atakaoacha kuvuta sigara!''

Ningewasihi wale wote wanaovuta sigara wafanye maamuzi kama hayo kwaajili ya kunusuru mapafu na afya yao wenyewe'' alisema Thomas.

Profesa Sally Davies, ambaye ni afisa mkuu wa matibabu,nchini Uingereza aliongeza kusema kuwa : "COPD ni ugonjwa mbaya licha ya kuwa haujulikana sana''.

"Jambo la busara kwa mvutaji sigara ni kutathmini afya ya mapafu yake mapema kisha kuchukua hatua zinazohitajika za kitabibu ilikunusuru maisha yao ikiwa ni pamoja na kuacha uvutaji wa sigara.''