Marekani yalipongeza jeshi la Iraq

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wakilinda mji wa Ramadi

Marekani imelipongeza jeshi la Iraq kwa kuweza kuurejesha mji wa Ramadi uliokuwa ukishikiliwa na wapiganaji wa Islamic State.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ash Carter amesifu hatua hiyo kwa kusema ni muhimu katika kulishinda kundi hilo, aliloliita kuwa ni la kishenzi.

Amesema ni muhimu pia kwa mamlaka za Iraq kwa kupata fursa ya kudhibiti amani katika mji huo wa Ramadi na kudhibiti kurudi tena kwa kundi hilo la IS.

Mwandishi wa BBC aliyetembelea mji huo wa Ramadi anasema majeshi ya serikali ya Iraq yanaendelea kuwasaka wapiganaji wa Islamic State waliosalia katika maeneo mbalimbali ya mji huo.