Wachimba migodi wapatikana hai China

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachimba migodi wapatikana hai China

Wachimba migodi wanane waliokwama ardhini kwa siku tano huko China wamepatikana wakiwa hai.

Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa makundi ya waokoaji bado hawajafanikiwa kuwaondoa chini ya ardhi ila wamewasiliana nao na kutuma vifaa na vyakula.

Wachimba migodi hao waliwaambia waokoaji kuwa walikuwa wamekwama katika njia za chini kwa chini.

Waokoaji ambao walikuwa wametupa camera ardhini walifurahia kuwapata hai wachimba migodi hao.

Wakati huohuo mkasa wa awali wa kuporomoka kwa timbo la mawe na vifusi vya ujenzi ulisajiliwa na vipimo vya tetemeko ya ardhi.

Wachimba migodi tisa bado hawajulikani waliko.

Saba waliokolewa mapema na moja anafahamika kuaga dunia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mawe yaliporoka kwenye mgodi huo ulio mkoa wa mashariki wa Shandong.

Mawe yaliporoka kwenye mgodi huo ulio mkoa wa mashariki wa Shandong.

Ripoti zinasema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea mmiliki wa mgodi huo alijiua wa kujirusha ndani ya kisima.

China inahistoria ndefu ya mikasa ya timbo na migodi inayolaumiwa kwa utepetevu wa idara za serikali kuhakikisha sheria na kanuni za afya na usalama zinazingatiwa na kutekelezwa na wamiliki wa migodi.