Facebook yashtakiwa kwa kuhodhi taarifa za fedha

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Facebook yashtakiwa kwa kuhodhi taarifa za fedha

Kampuni ya mtandao wa kijamii ya Facebook inakabiliwa na mashtaka mawili ya ukiukaji wa haki za wawekezaji wake ilipowanyima maelezo kamili kuhusiana na hisa zake mwaka wa 2012.

Hakimu wa mahakama ya juu ametoa idhini ya kesi hiyo inayowekwa na wenye hisa wanaodai walipoteza mamilioni ya pesa zao waliponunua hisa za kampuni hiyo kwa gharama ya juu kuliko mapato yake.

Hakimu tayari ametoa idhini wafungue mashtaka kwa makundi.

Facebook imeiambia BBC kuwa hairidhishwi kamwe na uamuzi huo wa mahakama na kuwa itakata rufaa.

Mgao wa kwanza wa hisa kwa umma mwezi Mei 2012 ulinasa dola bilioni $16.

Wawekezaji wanasema kwamba walinunua hisa ya kampuni hiyo kwa bei ya juu na kupoteza pesa zao bei ya hisa ilipoporomoka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mgao wa kwanza wa hisa kwa umma mwezi Mei 2012 ulinasa dola bilioni $16.

Toleo la kwanza liligharimu dola $38 hata hivyo kufikia mwezi Septemba hisa hizo zinauzwa kwa takriban nusu ya bei hiyo yaani dola $17.55 .

Wenye hisa wanalalamika kuwa kwa zaidi ya mwaka mmoja hisa za kapuni hiyo zilikuwa zinauzwa kwa tariban nusu ya bei waliyonunua na kuwaletea hasara maradufu.

Hata hivyo bei ya hisa hizo za kampuni ya Facebook zinauzwa kwa dola $107.26 kwenye soko la hisa la Nasdaq.

Jaji Robert Sweet aliidhinisha mashtaka hayo Desemba, tarehe 11.

Facebook hata hivyo imeiambia BBC kuwa mashtaka hayo hayana tija ikizingatiwa kuwa ilitoa takriban kura sa 55 ya maelezo ya jinsi matumizi ya simu yataathiri uwezo wa kupata faida wa kampuni hiyo.