Buhari: Niko tayari kushauriana na Boko Haram

Chibok Haki miliki ya picha AFP
Image caption Buhari amesema yuko tayari kushauriana na Boko Haram kuhusu wasichana waliotekwa Chibok

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema yuko tayari kushauriana na Boko Haram kuhusu kuachiliwa kwa wasichana 200 waliotekwa nyara karibu miaka miwili iliyopita.

Kiongozi huyo amesema yuko tayari kuondoa masharti yaliyokuwa yamewekwa kabla ya mazungumzo na wapiganaji hao wa Kiislamu kuanza.

Kwenye mahojiano katika runinga, Rais Buhari amesema mashauriano hayo yatategemea kuaminika kwa viongozi wa kundi hilo ambao watateuliwa kushiriki.

Amesema kufikia sasa hana habari za kijasusi kuhusu walipo wasichana hao kutoka mji wa Chibok, na hali yao kiafya.

Haki miliki ya picha

Boko Haram waliwateka wasichana hao kutoka mabweni ya shule mashariki mwa Nigeria miezi 20 iliyopita.