Wachunguzi watafuta chanzo cha moto Dubai

Moto Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafisa wanasema moto ulianza ghorofa ya 20 upande wa nje na haukusambaa ndani ya hoteli

Wachunguzi mjini Dubai wanajaribu kubaini chanzo cha moto uliozuka katika hoteli ya kifahari mkesha wa Mwaka Mpya na kujeruhi watu kadha.

Moto huo ulizuka katika ya kulipuliwa kwa fataki za kuukaribisha mwaka kwenye hoteli ya Address Downtown yenye ghorofa 63.

Watu waliokuwemo kwenye jumba hilo waliondolewa upesi.

Watu 16 hata hivyo wanaripotiwa walijeruhiwa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ulipuaji wa fataki Burg Khalifa uliendelea kama ilivyopangwa

Wazima moto walijaribu usiku kucha kuzima moto lakini kufikia asubuhi moshi ulikuwa bado unafuka.

Kulipuliwa kwa fataki katika jumba la Burg Khalifa, jengo refu zaidi duniani, uliendelea kama ilivyopangwa, mita mia kadha kutoka eneo la tukio.