Arsenal, Man Utd wang’aa EPL

Wayne Rooney Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wayne Rooney amefungia Man Utd bao la ushindi

Arsenal wamefungua mwanya wa alama mbili kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuandikisha ushindi dhidi ya Newcastle, Manchester United nao wakipanda kwa ushindi dhidi ya Swansea City.

Arsenal walilaza Newcastle 1-0, bao lao wakifungiwa na Laurent Koscielny kipindi cha pili, na kufikisha alama 42.

Leicester City wanaowafuata Arsenal walipoteza nafasi ya kujiimarisha baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Bournemouth, licha ya Bournemouth kucheza mwishoni mwa mechi na wachezaji 10 baada ya Simon Francis kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo mshambuliaji Jamie Vardy.

Riyad Mahrez alishindwa kuwafungia penalti

Uwanjani Old Trafford, ni shangwe kwa meneja Louis van Gaal baada ya vijana wake kuandikisha ushindi wa 2-1, mabao yao mawili wakifungiwa na Anthony Martial na nahodha Wayne Rooney.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Arsenal wamo alama mbili mbele ya Leicester

Kwingineko, Southampton walilazwa 1-0 ugenini Norwich City, bao hilo likifungwa baada ya kiungo wa kati wa Southampton kutoka Kenya Victor Wanyama kupewa kadi nyekundu.

Uwanjani Stadium of Light, Sunderland wamelaza Aston Villa 3-1.

Katika mechi ya awali, Liverpool walilazwa 2-0 na West Ham.

Matokeo kamili:

  • West Ham 2-0 Liverpool
  • Arsenal 1 -0 Newcastle
  • Leicester 0-0 Bournemouth
  • Man Utd 2-1 Swansea
  • Norwich 1 -0 Southampton
  • Sunderland 3-1 Aston Villa
  • West Brom 2-1 Stoke