Chris Brown atuhumiwa kumpiga mwanamke

Brown Haki miliki ya picha Getty
Image caption Brown alikiri makosa ya kushambulia Rihanna mwaka 2009

Polisi katika jiji la Las Vegas, Marekani wanachunguza madai kwamba mwanamuziki mashuhuri wa R&B Chris Brown alimpiga mwanamke Jumamosi.

Mwanamke huyo anadai msanii huyo alimgonga usoni alipojaribu kumpiga picha.

Kisa hicho kinadaiwa kutokea katika hoteli alimokuwa Chris Brown mapema Jumamosi asubuhi.

Mwanamuziki huyo hajazungumza lolote kuhusiana na madai hayo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Chris Brown na Rihanna walikuwa wapenzi

Mwaka 2009, Brown aliagizwa kukaa miaka mitano bila kufanya kosa baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga nyota wa muziki wa pop Rihanna.