Wagombea urais wapinga uchaguzi CAR

Haki miliki ya picha

Wagombea wa uraisi 20 kati ya 30 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wametoa wito wa kura zilizopigwa kufutwa kwa madai ya kuwepo kwa ulaghai.

Matarajio yalikuwa baada ya uchaguzi huo wa Jumatano wiki iliyopita kwamba hali ya amani ingeweza kurudi nchini humo ambako maelfu wamefariki dunia katika vita vya kidini.

Kura zaidi ya robo zimehesabiwa na Waziri mkuu wa zamani Faustin Archange Touadera, ndiye anayeongoza kwa sasa.

Msemaji wa kundi la wagombea hao 20, Théodore Kapou, amewaambia waandishi wa habari kuwa hawaridhishwi na jinsi uchaguzi huo uliendeshwa. "Sisi, wagombea kwa uchaguzi wa urais, watia sahihi wa tamko hili, tunakataa ushirika wa uchaguzi batili kama huu.Tunatangaza kuwa mchakato wa uchaguzi si wa kuaminika. Ni lazima usimamishwe ili ushirikiano uwepo na utekelezwaji uendele."