Serikali ya Burundi kususia mazungumzo Arusha

Mazungumzo Haki miliki ya picha Getty
Image caption Serikali ya Burundi inasema hakukuwa na maafikiano kuhusu tarehe ya kuanza mazungumzo

Serikali ya Burundi imesema haitashiriki mazungumzo ya amani ambayo yamepangiwa kuanza hapo kesho mjini Arusha, Tanzania.

Mazungumzo hayo ni matokeo ya mazungumzo yaliyofanyika nchini Uganda chini ya uongozi wa Rais Yoweri Museveni.

“Hakuna mazungumzo kesho au hata 16 Januari kama wengi wanavyodhani, kwa sababu hakujakuwa na maafikiano kuhusu tarehe hiyo,” katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje wa Burundi Joseph Bangurambona ameambia shirika la habari la Reuters.

Machafuko yalianza Burundi Aprili mwaka jana baada ya Rais Nkurunziza kutangaza angewania urais kwa muhula wa tatu.

Visa vya watu kuuawa vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara mjini Bujumbura.