Wahamiaji 17 wafa maji wakielekea Uturuki

Wahamiaji Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wahamiaji hao walikuwa wameabiri boti mbili

Wahamiaji 17 wamekufa maji baharini muda mfupi baada yao kutoka Uturuki wakielekea Ugiriki.

Wahamiaji hao walikuwa kwenye boti mbili ambazo inaaminika zilizama wahamiaji hao walipokuwa wakivuka bahari kufika kisiwa cha Lesbos.

Miili yao imesombwa na maji na imepatikana kwenye ufukwe wa Ayvalik na Dikili eneo umbali wa maili 30.

Zaidi ya wahamiaji milioni moja walivuka bahari mwaka wa 2015 na wengi wao walitoka Uturuki kuelekea Ugiriki.

Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa wahamiaji 3,771 waliokuwa wamefunga safari ya kuelekea Ulaya hawajulikani waliko.

Hali ya hewa katika bahari ya Aegean hii leo imekuwa mbaya na maafisa wamesema wahamiaji hao walikuwa wanatumia vihori vya raba kufika Lesbos.

Kulingana na shirika la habari la Dogan ,Walinzi wa pwani ya Ayvalik wamewaokoa watu wanane.

Igawa uraia wa waliozama bado haijabainishwa, Gavana Namik Kemal Nazli Hurriyet amesema walikuwa raia wa syria, Iran na Algeria.

Siku ya jumapili wahamiaji kadhaa waliokolewa kutoka kwa kisiwa kidogo karibu na mji wa Dikili, wakielekea kisiwa cha Lesbos.