Wanawake 90 wabakwa Ujerumani mwaka mpya

Wanawake Haki miliki ya picha .
Image caption Wanawake hao wanadaiwa kunyanyaswa kingono na watu wa asili ya Uarabuni au Afrika Kaskazini

Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel, ameshtushwa na madai kwamba wanawake wapatao 90 walinyanyaswa kingono wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 mjini Cologne.

Polisi pamoja na mashuhuda wa matukio hayo wameelezea mashambulio hayo ya kingono kuwa yalitekelezwa karibu na eneo maarufu la Cathedral, ambalo lilikuwa limefurika idadi kubwa ya makundi ya wanaume wenye asili na muonekano wa Kiarabu ama Afrika Kaskazini.

Merkel ametoa agizo la kufanyika uchunguzi wa kubainiukweli kuhusiana na madai hayo na kisha kuwaadhibu wahusika, bila kujali asili yao ama historia za awali.

Meya wa mji wa Cologne, Henriette Reker, ameonya juu ya hatua zitakazochukuliwa akisa haki inafaa kutendeka bila ya kuwaelemea wakimbizi walioingia nchini Ujerumani.

Ameitisha mazungumzo ya dharura na maafisa wa polisi kuhusiana na mgogoro huo.

Polisi wameahidi kuimarisha ulinzi.