Zimbabwe kuuzia China wanyamapori wengi

Ndovu wa Zimbabwe Haki miliki ya picha b
Image caption Uchina itaweza kuuziwa ndovu kutoka Zimbabwe

Zimbabwe itaongeza idadi ya wanyamapori ambao inauizia taifa la Uchina, wanyama hao ni pamoja na ndovu.Hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Mazingira Oppah Muchinguri.

Waziri huyo amesema kuna hatari ya ndovu kuangamia kutokana na kiangazi.Hata hivyo wakosoaji wametaja hatua hiyo kama uporaji wa raslimali za vizazi vijavyo vya taifa hilo.

Zimbabwe pia inanuia kupata msaada wa China kupata teknolojia ya kukabiliana na ujangili,ikiwemo kupata ndege zisizokuwa na rubani kuwawinda majangili.

Image caption Wanyamapori wengi wanakabiliwa na kiangazi ambazo kimekumba Zimbabwe

Mbuga za wanyama pori nchini Zimbabwe ni maarufu sana kwa watalii, lakini wanyama pori wameendelea kukabiliwa na wawindaji haramu ambao soko lao kubwa ni China na mataifa kadhaa ya Bara Asia.

Zimbabwe pia inakabiliwa na matatizo ya kifedha kiasi cha kushindwa kusimamia mbuga zake.Maafisa wa serikali wanaamini kuuza wanyamapori nchini China kutasaidia kupata fedha za uhifadhi wa wanyamapori wengine watakaobakia ndani ya mbuga.

Tangu mwaka jana Zimbabwe imeuza ndovu 100 kwa China kati ya idadi ya sasa ya ndovu 84,000.