Kocha wa Leicester akiri makosa

Ranieri Haki miliki ya picha AP
Image caption Leicester City kwa sasa wamo nambari mbili EPL

Meneja wa Leicester City Claudio Ranieri amekubali makosa ya kuendesha gari kwa kasi isiyoruhusiwa eneo la Cambridgeshire na akapigwa faini.

Ranieri, 64, anayekaa Leicester, alinaswa akiendesha gari kasi ya maili 96 kwa saa eneo lisiloruhusiwa mtu kupita kasi ya maili 70 kwa saa mwezi Oktoba.

Amekiri kosa hilo na akapigwa faini ya £700 katika mahakama ya hakimu eneo la Peterborough.

Aliwakilishwa na wakili wake.

Ranieri pia amewekewa alama tano za kufanya makosa katika leseni yake na akatakiwa kulipa gharama ya kesi ya £85 na nyingine £70.

Klabu inayokufunzwa na Mwitaliano huyo kwa sasa imo nambari mbili katika Ligi ya Premia.

Amewahi kuwa mkufunzi wa Chelsea na Juventus miongoni mwa timu nyingine, na pia timu ya taifa ya Ugiriki.