Mshukiwa mkuu wa mihadarati akamatwa Mexico

Haki miliki ya picha AP
Image caption Afisa wa polisi akimsaka Guzman el Chapo katika mtaru wa maji chafu nchini Mexico

Mmoja wa walanguzi wakuu wa mihadarati nchini Mexico "El Chapo" Guzman amekamatwa baada ya kuwa mafichoni kwa miezi sita.

Alikamatwa na polisi katika hoteli moja na mmoja wa washirika wake viungani mwa mji wa Los Mochis katika jimbo la Sinaloa, ambalo ni kituo kikuu cha harakati za mifumo ya biashara za mihadarati.

Alitoroka uvamizi wa asubuhi kupitia mtaro, lakini alikamatwa na kikosi cha wanamaji alipokua akijaribu kutoroka kwenye gali lake.