Nchi za kiarabu kufanya kikao cha dharura

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Viongozi wa mataifa ya kiarabu wakikutana katika mkutano wa siku za nyuma

Kikao cha dharura cha mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya kiarabu kitafanyika hii leo mjini Cairo.

Kikao hicho kimeitishwa na Saudi Arabia kufuatia shambulizi dhidi ya ubalozi wake nchini Iran, baada ya Saudi Arabia kumuua mhubiri wa kishia.

Mwandishi wa BBC anasema huenda mwafaka usiafikiwe, kwani mataifa kama Iraq na Lebanon huwa chini ya ushawishi wa Iran, na pia washirika wa karibu wa Saudi Arabia hawajaiunga mkono Saudia kikamilifu.