Twitter kuongeza idadi ya herufi hadi 10,000

Haki miliki ya picha PA
Image caption Twitter

Twitter ina mpango wa kuongeza kiwango cha idadi ya herufi zinazoandikwa katika nafasi ya ujumbe kutoka 140 hadi 10,000 sawa na ujumbe wa kawaida.

Baada ya saa 24 za uvumi mtandao huo sasa umeamua kuongeza idadi hiyo.

Ni hatua ya hivi karibuni ya Twitter kuweza kuwavutia wateja zaidi.

Mkuu wa Twitter na mwanzilishi Jack Dorsey amesema kuwa ataongeza idadi ya kiwango cha herufi zitakazotumika.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwanzilishi wa Twitter Jack Dorsey

Iwapo Twitter itakubali kiwango cha ujumbe wenye herufi 10,000 huenda ikazalisha ujumbe wa maneno 1,700.

Katika ujumbe wake ,Jack Dorsey ameandika kwamba Twitter tayari imebaini kwamba wengi wa wateja wake milioni 300 tayari wamekuwa wakipiga picha kubwa za ujumbe mrefu katika ujumbe wao.

Amesema kuwa Twitter inajaribu kutafuta mbinu za kuwapa watu zaidi uwezo wa kujielezea bila kuchafua huduma hiyo.