Mwandani wa Buhari arejesha 'fedha za wizi'

Image caption Isa Lawal

Mshirika wa karibu wa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amerejesha dola laki tano ambazo anadaiwa kupokea kutoka kwa aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama nchini humo Sambo Dasuki kulingana na gazeti la Daily Trust nchini humo.

Lawal Jafaru Isa,mmoja wa viongozi wa chama tawala cha All Progressive Congress,alikamatwa wiki iliopita katika uchunguzi wa dola bilioni 2 za ununuzi wa vifaa vya kijeshi ili kulikabili kundi la wapiganaji wa Boko Haram ,ambazo zilitoweka wakati wa uongozi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Goodluck Jonathan.

Bwana Isa alikuwa mtu wa karibu wa Bwana Buhari kukamatwa kuhusiana na kashfa hiyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Alituhumiwa kupokea dola lakini nane na hamsini kutoka kwa bwana Dasuki.

Vyombo vya habari vya eneo hilo vimeripoti kwamba ameachiliwa baada ya kuahidi kurudisha kitita cha dola laki tatu na hamsini zilizosalia.

Bwana Isa amesema kuwa alipewa fedha hizo kumnunulia nyumba bwana Dasuki na kwamba hakujua fedha hizo zilitoka kwa serikali.

Haki miliki ya picha
Image caption Sambo Dasuki

Bwana Dasuki hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo ya bwana Isa lakini amesisitiza kuwa hakufanya kosa lolote.

Bwana Dasuki ambaye ni mwandani wa karibu wa aliyekuwa rais wa taifa hilo,ameshtakiwa kwa madai ya kuzipeleka ,mahala kwengine fedha za serikali.

Amekana kutekeleza makosa hayo.

Viongozi kadhaa wa upinzani wanakabiliwa kuhusu ufisadi huo.

Takriban watu 17,000 wameuawa kaskazini mashariki mwa Nigeria wakati wa mashambulizi ya miaka sita ya kundi la boko haram ili kubuni serikali ya kiislamu.