Mawakili wagoma Niger

Image caption Ras Mahamadou Issoufou amelaumiwa kwa ukandamizaji

Mawakili nchini Niger wameanza mgomo wa sasa 24 kupinga kile wanachokitaja kuwa kukamatwa wa wapinzani wa serikali na hatua ya serikali ya kuwazuia kukutana na wateja wao.

Kukamatwa huku kunajiri baada ya rais Mahamadou Issoufou mwezi uliopita kuwalaumu maafisa wa vyeo vya juu jeshini kwa kujaribu kuipindua serikali yake.

Upinzani na mashirika ya umma yamelalamika kwa kukandamizwa tangu yafanyike majaribio ya mapinduzi yanayodaiwa.

Kuna msukosuko mkubwa nchini Niger kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa urais mwezi ujao, ambapo rais Issoufou anawania muhula wa pili.

Rais Issoufou yuko katika nafasi nzuri ya kushinda lakini wakosoaji wanasema kwa amekuwa mkandamizaji kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.