Mawakili 7 wa haki za kibinadamu wakamatwa

Image caption Zhou Shifeng

Maafisa nchini Uchina wamewatia mbaroni zaidi ya mawakili 7 wa haki za kibinadamu, ambao walikuwa wametoweka tangu mwezi Julai.

Mawakili hao wameshtakiwa kwa makosa ya uchochezi.

Saba hao ni miongoni mwa mawakili 140 waliotiwa mbaroni na maafisa wa usalama nchini humo, na kuwekwa kwenye kizuizi cha siri.

Walikuwa wafanyikazi wa kampuni ya sheria ya Fengrui mjini Beijing, ambayo iliwakilisha familia za waathiriwa wa sakata ya maziwa ya watoto yaliyotiliwa sumu mwaka wa 2008.