Ujerumani yarudisha wahamiaji Austria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ujerumani yarudisha wahamiaji Austria

Ujerumani imekuwa ikipeleka wahamiaji kadha kwenda Austria kila siku tangu mwanzo wa mwezi huu kwa mujibu wa polisi nchini Austria.

Wengi hawakuwa na stakabadhi halali huku wengine hawakuwa na mpango wa kuomba hifadhi nchini Ujerumani lakini nchi zingine hasa za Scandinavia.

Mashambulia ya mwaka mpya dhidi ya wanawake mjini Cologne ambapo wahamiaji walilaumiwa yametoa shinikizo kali kwa chansellor wa ujerumani Angela Merkel. Wengi wa wale walipelekwa nchini Austria si raia wa Syria.

Image caption Wengi hawakuwa na stakabadhi halali

Wao ni wahamiaji wengi kutoka nchini Afghanistan, Morocco na Algeria.

Mapema ripoti rasmi zilisema kuwa wanaume wanaokisiwa kuwashambulia wanawake mjini Cologne wana historia ya wahamiaji hasa kutoka kaskazini mwa Afrika na nchi za kiarabu.