Waisrael wanne washtakiwa kwa mauaji

Haki miliki ya picha Olivier Fitoussi
Image caption Miongoni mwa Waisrael wanaokamatwa kwa kuchukua sheria mkononi

Waisrael wanne wameshtakiwa kwa kuhusika na kumpiga mhamiaji kutoka Eritrea, ambaye alidhaniwa kuwa mpiganaji wa kiarabu.

Habtom Zerhom alikuwa katika kituo cha basi wakati Mpalestina mmoja aliposhambulia na kumuua askari wa Israel.

Walinzi wa Usalama waliokuwepo kwenye shambulio hilo walimdhania mhamiaji huyo wa Eritrea kuwa naye pia ni mshambuliaji, hivyo wakampiga risasi.

Baada ya kudondoka kutokana na majeraha aliyoyapata huku akivuja damu, kundi la watu wenye hasira pia lilimshambulia.

Mhamiaji huyo kutoka Eritrea alifariki dunia baadaye kutokana na majeraha aliyoyapata.