Waandamana kupinga wahamiaji

Haki miliki ya picha Getty

Maelfu ya waandamanaji wamefanya mkutano katika mji wa Leipzig Kupinga wahamiaji.

Waandamanaji hao wanaopinga waislamu wanalaumu kuingia kwa wingi kwa wahamiaji kunasababisha ongezeko la udhalilishaji wa kijinsia na ujambazi unaolenga wanawake.

Wamemtolea hasira zao Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye wanamlaumu kwa kile walichoita kuiteketeza nchi yao kwa kuruhusu wahamiaji zaidi ya milioni mwaka uliopita.

Maafisa nchini humo wanasema wengi waliohusika na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia wakati wa mkesha wa mwaka mpya asili yao ni wahamiaji.