UN wakuta hali mbaya Madaya,Syria

Image caption Magari ya Umoja wa mataifa UN,yakipeleka misaada

Mratibu wa msafara wa kutoa misaada katika mji wa Madaya nchini Syria, Yacoub El Hillo amesema wameowaona watoto wakiwa katika hali mbaya kutokana na kukosa chakula.

El Hillo ameongeza kuwa picha zilizopigwa awali zikionyesha wakazi wa maeneo hayo wakiwa katika hali mbaya kwa kukosa chakula ni za kweli kabisa na ni sawa na kile walichokishuhudia baada ya kufika eneo hilo.

Misaada ya chakula na dawa imepelekwa pia kwenye vijiji viwili kaskazini mwa Syria ambavyo vinaunga mkono Serikali na ambavyo vimeathirika kutokana na mashambulizi dhidi ya waasi.

Naye balozi wa umoja wa mataifa wa Syria Bashar Al Jaafari, amekaririwa akidai kuwa shida katika mji wa madaya imesababishwa na upande wa waasi.

Taarifa kuhusiana na hali ya kibinadamu Madaya ni matokeo ya taarifa za uongo na upuuziaji wa vitendo vibaya vinavyotokea katika maeneo mengine ambayo yanashambuliwa na makundi ya waasi.

Ukweli wa mambo kwa kile kinachoitwa mapigano ni kwamba katika baadhi ya maeneo waasi wanawatumia raia kama kinga yao”

Hata hivyo baadhi ya wanadai pia kuwa waasi wamehifadhi chakula kwaajili ya familia zao na wamekuwa wakiuza ziada ya chakula hicho kwa kiwango kikubwa ambacho ni Zaidi ya dola 400 kwa kilo moja ya mchele.

Serikali ya Syria imekanusha madai ya kwamba inatumia uhaba wa chakula kama moja ya mbinu za kivita.