Nigeria kurudisha fedha zilizoibiwa

Image caption Rais Muhammadu Buhari ameweka kipaumbele vita dhidi ya ufisadi

Serikali ya Nigeria inasema kuwa iko kwenye mazungumzo na Uswisi kuhusu kurejeshwa kwa dola millioni 300 za Kimarekani zilizoibiwa na kiongozi wa zamani wa kijeshi Sani Abacha.

Waziri wa mashauri ya kigeni Geoffrey Onyeama alisema kuwa dola millioni 700 za Kimarekani tayari zimerudishwa kutoka nchini Uswisi.

Shirika la Transparency International linamlamu Sani Abacha kwa kuiba hadi dola billioni tano wakati alikuwa madarakani kati ya mwaka 1993 hadi mwaka 1998.

Rais Muhammadu Buhari ameweka kipaumbele vita dhidi ya ufisadi na kuzitaka Uingereza na Marekani kusaidia kurudisha fedha zilizoibiwa.