Radcliffe apinga kufutwa kwa rekodi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwanariadha mkongwe wa Uingereza Paula Radcliffe.

Mwanariadha mkongwe wa Uingereza Paula Radcliffe amesema mapendekezo yaliyotolewa na shirikisho la mchezo wa riadha nchini Uingereza, UKA ya kufutilia mbali rekodi zote za riadha, itakuwa sawa na kuwaadhibu wanariadha wasiokuwa na hatia.

UKA, imetoa mapendekezo 14 ikiwemo kutoa adhabu ya marufuku ya muda mrefu kwa wanariadha watakaopatikana na hatia ili kuashiria mwanzo mpya.

Radcliffe aliweka rekodi ya ulimwengu ya mbio za kina dada za masafa marefu za marathon mjini London mwaka wa 2003.

''Kamwe sitakubali rekodi za dunia kufutiliwa mbali kwa sababu nina uhakika wa asilimia mia moja kuwa baadhi ya rekodi hizo ziliwekwa na wanariadha ambao hawajawahi kutumia madawa ya kusisimua misuli, na hilo ndilo jambo muhimu zaidi'' Radcliffe aliliambia gazeti la the Guardian.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Radcliffe aliweka rekodi ya ulimwengu ya mbio za kina dada za masafa marefu za marathon mjini London mwaka wa 2003.

Ameongeza kusema kuwa endapo pendekezo hilo litaidhinishwa basi itakuwa pigo kwa wanariadha watiifu na kuwa haitakuwa na maana kwa sababu wanariadha hao watashindana tena na wale waliopatikana na hatia katika mashindano yajayo.

Mchezo wa riadha umekumbwa na madai ya kuwepo kwa visa vingi vya utumizi wa madaway ya kusisimua misuli pamoja na ulaghahi wa kujaribu kuwakinga wanariadha waliopatikana na hatia.

Urussi imepigwa marufuku ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa baada ya serikali ya nchi hiyo kutuhumiwa kufadhili na kuhimizi wanariadha wake kutumia madawa hayo yaliyoharamishwa.

Sehemu ya pili ya ripoti hiyo ya WADA inatarajiwan kuangazia sana shirikisho la mchezo wa riadha duniani IAAF, hasa kufuatia madai ya kuhusika na njama ya ufisadi na kujarbu kuficha ukweli kuhusu sakata hiyo.