Kesi ya naibu rais wa Kenya yaendelea

Image caption Wakili wa Ruto Karim Khan

Kesi ya uhalifu inayomkabili naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ya The Hague hatimaye imeanza.

Ruto yuko katika mahakama hiyo na mwandishi Joshua Arap Sang ambaye pia anajaribu kutoa ushahidi utakaosababisha kufutiliwa mbali kwa kesi hiyo inayohusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Mnamo mwezi Disemba mwaka jana mahakama hiyo ilifutilia mbali mashtaka dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa ukosefu wa ushahidi,lakini mwendesha mashtaka anahoji kwamba bwana Ruto na mwandishi Joshua Sang wana kesi ya kujibu.

Washtakiwa wanasema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea huku wakikana mashtaka hayo.