Maambukizo ya Ebola Afrika kutokomezwa

Haki miliki ya picha AP

Shirika la Afya Duniani leo linatarajiwa kutangaza kuisha kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Liberia.

Liberia ni nchi ya mwisho iliyokuwa ikipambana na maambukizi hayo.

Na kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka miwili ya mlipuko huo, nchi zote zilizoathirika zimeweza kudhibiti kuendea kwa maradhi hayo.

Liberia hii leo imekamilisha siku arobaini na mbili tangu watu wa mwisho waliotibiwa na kupona kutokana na Ebola kupatikana bila virusi hivyo.

Katika mlipuko huo mkubwa zaidi wa Ebola, watu zaidi ya 28,000 waliambukizwa na miongoni mwao 11,000 walifariki.