14 wauawa kwenye kituo cha chanjo Pakistani

Polisi pakistan Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi katika mji wa Quetta nchini Pakistani baada ya mlipuko wa bomu kwenye eneo la tukio

Takriban watu 14 wameuawa katika shambulio la bomu nje ya kituo cha kutoa chanjo ya ugonjwa wa kupooza(polio) katika mji wa kusini magharibi wa Quetta nchini Pakistani, kwa mujibu wa maafisa.

Wengi miongoni mwa waliouawa wanadhaniwa kuwa ni polisi waliokuwa wakilinda kliniki.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanamgambo wa Islamic State wamekua wanasema chanjo za kupooza zinazuia uzazi nchini pakistani

Polisi wenye silaha huwalinda wahudumu wa afya wanaotoa chanjo ya kupooza nchini Pakistani ambao wamekua wakilengwa na mashambulio mabaya ya Islamic State miaka ya hivi karibuni.

Wanamgambo wa Islamic State wanapinga chanjo ya kupooza , wakisema ni mpango wa nchi za magharibi wa kufunga uzazi dhidi ya watoto wa Pakistani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Pakistan na Afghanstan ndio nchi pekee zenye maambukizi mengi ya maradhi ya kupooza zaidi duniani

Pakistan na Afghanistan ni nchi pekee zilizosalia zenye visa vingi vya marathi ya kupooza.

Mlipuko wa bomu hilo ulitokea mapema subuhi wakati wahudumu wa kutoa chanjo na maafisa wa usalama walipokua wakiripoti kazini kabla ya kuelekea nje kwa mizunguko ya kutoa chanjo hiyo , amesema Sarfaraz Bugti, waziri katika jimbo la Balochistan ambalo Quetta ni mji mkuu wake.

Polisi katika eneo hilo wanasema kuwa mlipuko huo uliwauwa polisi 12, mwanajeshi mmoja na raia mmoja. Watu wapao 20 wamejeruhiwa.