Google yasema magari yake ni Salama

Haki miliki ya picha AP
Image caption Google inataka kujenga magari yasiyo na vidhibiti ambayo vinatumika hivi sasa kwa magari mengine

Madereva wa magari yanayojiendesha ya Google walilazimika kushika usukani wa magari hayo ili kuzuia yasifanye ajali katika barabara za Carlifonia mara 13 kati ya mwezi Septemba mwaka 2014 na Novemba mwaka 2015.

Ufichuzi huo unatolewa baada ya wasimamizi kutaka kupata habari kamili kuhusu magari hayo.

Makampuni mengine sita ya teknolojia ya magari pia yalifichua taarifa kuhusu visa vya usalama vya magari hayo yanayojiendesha.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Google inasema magari yake yaliejiendesha zaidi ya umbali ya maili 230,000 bila ya kutokea kwa kisa chochote cha ajali

Google inataka kujenga magari yasiyo na vidhibiti ambayo vinatumika hivi sasa kwa magari mengine, lakini shirika linalofuatilia usalama wa bidhaa katika jimbo la Carlifonia linasema kuwa taarifa hizo zinahujumu mradi huo.

Googe inasema kuwa visa kama hivo vya ajali ni vichache na waaandisi wao wanajitahidi kuhakikisha kuwa magari yanayojiendesha yamefanya kazi inavyotakiwa na kwa usalama.

Inasema kuwa tangu mwezi Aprili mwaka 2015 , magari yake yaliejiendesha zaidi ya umbali ya maili 230,000 bila ya kutokea kwa kisa chochote cha ajali.