Mugabe 'hajapatwa na mshtuko wa moyo'

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ana miaka 91

Uvumi kuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 91 amepata mshutuko wa moyo ni uongo mtupu.

Hii ni kwa mujibu wa msemaji wake George Charamba ambaye amenukuliwa na gazeti la serikali la Herald.

Mtandao wa habari wa Zim Eye ulisema jana kuwa Bw Mugabe anaaminiwa kuanguka baada ya kupata mshtuko wa moyo akiwa likizoni na familia yake.

Bw Charamaba aliliambia gazeti la the Herald kuwa hiyo ni mbinu ya mitandao kupata pesa.

Alisema kuwa kila Januari taarifa hujitokeza kuhusu kifo cha rais.